Rais Barack Obama wa Marekani
hatomuunga mkono wazi mgombea yeyote wa urais kabla ya chama cha
Democratic hakichamchagua mgombea atakayewania wadhifa huo ili
kuingia Ikulu Novemba.
Mkuu wa watumishi wa Ikulu ya
Marekani Denis McDonough, amesema rais Obama hatompigia kampeni
mgombea yeyote wa urais katika kipindi hiki cha kampeni za awali za kuwania
kuidhinishwa na chama.
Kura za maoni kwa upande wa chama
cha Democratic zinaonyesha Hillary Clinton anaongoza, akifuatiwa na
Seneta wa Vermont Bernie Sanders.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni