Watu wapatao wanne wameuwawa wakati
kombora lilipotua kwenye hospitali inayoungwa mkono na Shirika la
Madaktari Wasioa na Mipaka (MSF) kusini mwa Yemen, shirika hilo
limesema.
MSF wamesema shambulizi hilo katika
mkoa wa Saada, ambao ni ngome kuu ya waasi wa Houthi, limejeruhi pia
watu wengine 10.
Kundi la waasi la Houthi linapigana
na vikosi vya serikali pamoja na washirika wa Saudi Arabia.
Shirika la MSF limesema
haijafahamika iwapo hospitali hiyo imepigwa na kombora lililorushwa
na ndege ya Saudi na washirika wake ama kwa roketi iliyorushwa kutoka
aridhini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni