Serikali ya Gambia imepiga marufuku
wafanyakazi wanawake kuacha nywele zao wazi wakiwa kazini, kwa mujibu
wa gazeti moja lililonasa agizo hilo.
Agizo hilo la serikali limewataka
wanawake kufunika vyema nywele zao, ila hazikutolewa sababu za
kwanini wafanyakazi wanawake wanapigwa marufuku kuacha vichwa vyao
wazi.
Hata hivyo wanawake wa imani za dini
nyingine hawatoshurutishwa kufunika vichwa vyao wawapo kazini, ila
wanaweza kufanya hivyo kwa mapenzi yao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni