Ndege za shirika la KQ zilizokuwa
zitue uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini, Nairobi leo
asubuhi zimelazimika kuagizwa kwenda kutua Mombasa kutokana na hali
mbaya ya hewa.
Maafisa wamesema ndege hizo namba
KQ765, KQ499 na KQ552 zimelazimika kwenda kutua Mombasa kutokana na
kuwepo kwa ukungu mzito Jijini Nairobi.
Shirika la Ndege la Kenya Airways
limesema sasa ndege zimeanza kutua tena uwanja wa Kimataifa wa Jomo
Kenyatta kuanzia majira ya saa tatu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni