Wakili wa mchekeshaji mkongwe
Marekani Bill Cosby amesema shitaka la shambulio la ngono
linalomkabili mteja wake huyo linamsukumo wa kisiasa.
Akiongea katika kipindi cha runinga
wakili Monique Pressley amesema mwendesha mashtaka wa kesi hiyo
hataki haki ila anashinikiza kutimiza ahadi za kampeni.
Zaidi ya wanawake 50 wamemtuhumu
Cosby kwa kutumia dawa za kulevya pamoja na pombe na kisha
kuwadhalilisha kingono. Jumatano wiki hii alifunguliwa shtaka rasmi
la kwanza huko Pennsylvania.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni