Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha (kulia) akitoa taarifa fupi ya utendaji kazi wa jeshi hilo pamoja na mafanikio kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga alipotembelea makao makuu ya jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akipokea nyaraka kadhaa pamoja na taarifa fupi ya utendaji kazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji toka kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha katika ziara yake. |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na baadhi ya maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika ziara yake katika kituo kikuu cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam kuangalia vifaa na shughuli za jeshi hilo. |
Kituo cha kupokea taarifa za majanga ya moto cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam. |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akiwa katika Kituo Kikuu cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Ilala Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto Jesuald Ikonko akimuongoza. |
Hapa akipata maelezo toka kwa mafundi wa karakana kuu ya Jeshi la Zimamoto Ilala Dar es Salaam. |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga akipata maelezo ya namna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na jeshi hilo vinavyofanya kazi kwa baadhi ya vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga (kushoto) akipata maelezo ya namna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na jeshi hilo vinavyofanya kazi kwa baadhi ya vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. |
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya ziara yake katika ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. |
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni