.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 9 Januari 2016

WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA FINLAND NCHINI

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na balozi wa Finland nchini Mhe. Pekka Hukka kabla ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 8, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland nchini, Bwana Pekka Hukka.


Akizungumza na Balozi Hukka leo, alipomtembelea ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo kwa namna ambavyo nchi ya Finland imeendelea kuisaidia Tanzania na kumumwomba waendeleze uhusiano mwema uliokuwepo kwa zaidi ya miaka 50 sasa.

“Ninashukuru na kutambua mchango wa nchi yako wa kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali ikwemo Utalii na Biashara, ninashukuru sana kwa hilo” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.


Pia, alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka Finland kuja kuwekeza katika sekta ya viwanda na kuendeleza maeneo ya ukanda maalum ya uwekezaji (EPZ) ili kuongeza thamani ya mazao pamoja na kutatua tatizo la ajira nchini.

Waziri Mkuu, pia ameendelea kwa kusema Serikali imedhamiria kukusanya mapato kikamilifu na kuzuia mianya ya upotevu wake, hivyo ameiomba Serikali ya Finland isaidie katika kujenga uwezo wa namna bora zaidi ya utekelezaji wa dhamira hiyo, kwa kuwa Finland ni kati ya nchi zenye mifumo bora na madhubuti ya ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wake, Balozi Hukka amesema nchi yake kupitia Balozi za Tanzania na Finland zimeanza jitihada za kuandaa utaratibu kwa ajili ya kuwekeza nchini , na kuna baadhi ya kampuni tayari ziko nchini.

(Mwisho)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni