.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 2 Februari 2016

FASTJET YAONGEZA NDEGE YA TANO

                                                               Dar es Salaam, Januari 28, 2016-Fastjet
 

Tanzania imeongeza ndege nyingine aina ya Airbus A319 kwenye idadi ya ndege zake nne na hivyo kuliweka shirika hilo la ndege la gharama nafuu kuendelea na mipango yake ya kupanuka.

“Ndege za fastjet kwa hivi sasa ni nne na zote zinatumika na ongezeko la ndege ya tano ni jibu kwenye mikakati yetu ya kupanuka pamoja na hitaji la kuongeza uwezo wa kubeba kwenye safari zetu za ndani na za kimataifa”, alisema Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania, John Corse.

Ndege hiyo ya nyongeza inafanya jumla ya nafasi inayokuwepo kwa siku kwenye safari kwa ajili ya wateja kufikia 1,000.

Fastjet ilianza safari zake nchini mwaka 2012na hivi sasa inajiendesha kwa kutumia ndege tano aina ya A319 kwenye mtandao wake wa safari ambao unahusisha Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro na Zanzibar na kuifanya ijikite kuufanya usafiri wa anga ndani ya Tanzania watu wote waumudu.

Hali kadhalika ilianzisha safari za kimataifa kwenda Entebbe nchini Uganda, Nairobi Kenya, Harare Zimbabwe, Johannesburg Afrika Kusini na Lusaka nchini Zambia katika kipindi cha miaka mitatu ya kuendesha shughuli zake.

“Tangu tuanze safari zetu tumeshabeba abiria zaidi ya 1,800,000 ambapo utafiti wetu unaonesha kuwa zaidi ya theluthi moja ya abiria wetu walikuwa ndio mara yao ya kwanza kumudu kusafiri kwa ndege”, anasema Corse.

Aliendelea kusema, “kuongeza ndege nyingine kwenye safari zetu kunatupa fursa muhimu ya kuongeza masafa kwa njia zetu zilizopo ili kukidhi mahitaji ya wateja, na na inasaidia kwenye lengo letu la kuongeza njia moja ya kimataifa kwenye mtandao wetu kwa mwaka huu 2016”.

Hali kadhalika, Corse anabainisha kuwa ndege hiyo mpya inamanisha kuwa fastjet ni sawia na ni kubwa katika kutosheleza kupanuka kwa shughuli za fastjet.

Ndege hiyo A319 ambayo ni Airbus ni ya injini mbili ambazo zinatoa kiwango cha juu cha ufanisi pamoja na kiwango cha chini kabisa cha madhara kwenye mazingira, ikiwa ni nyongeza kwenye viwango vya juu vya hali ya kuliwaza ndani ya ndege hiyo ya kisiasa.

Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 156 ambaop wanamudu viwango vya chini vya kuendesha mtindo wa maisha wa gharama nafuu ambao unaendeshwa na Fastjet Tanzania.

Baadhi ya njia muhimu ambazo ndege hiyo mpya itakuwa inahudumia ni njia mpya iliyoanzisjhwa hivi karibuni kati ya Dar es Salaam na Nairobi, Kilimanjaro na Nairobi na Dar es Salaam kwenda Zanzibar ambazo zote zilianza kwa mara ya kwanza Januari 11, 2016. njia hizi mpya zote ni kielelezo muhimu muda mrefu kwenye upanuzi wa njia za fastjet kitaifa na kimataifa.

Fastjet inatarajia kuongeza ndege zaidi kwenye njia yake ya Kenya kutokana na mahitaji ya wateja kuongezeka kunakosababisha na kumudu, usalama, kasi na huduma kwa wakati, na hali kadhalika imeshajionesha kuwa kuna matarajio ya kuzindua safari kati ya Zanzibar na Nairobi na hali kadhalika kati ya Dar es Salaam na Mombasa baadaye mwaka 2016.

“Usafiri wa anga unaoumudu ni muhimu kwenye kukuza uchumi wa Tanzania, hususani kwenye kukuza sekta za biashara na utalii”, alisema Corse.

Hali kadhalika Corse alibainisha kuwa ndege hiyo mpya inamaanisha kwamba ndege za Fastjet zitatosheleza kiasi cha kutosha kusaidia kwenye changamoto za usimamizi na uendeshaji iwapo ndege moja miongoni mwake itakuwa haifanyi kazi au kama ipo kwenye matengenezo au ukarabati wa lazima.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni