Theluji kali imeathiri usafiri wa
umma kusini mwa China, na kukwamisha makumi ya maelfu ya watu nje ya
stesheni ya reli.
Polisi wamesema umati wa watu nje ya
stesheni ya Guangzhou umeongezeka na kufikia watu 100,000.
Eneo la kati la China linatarajia
kupata hali ya hewa ya baridi mno kuwahi kutokea kwa miaka mingi.
Theluji hiyo adimu imetokea wakati
nchi ya China ikiadhimisha mwaka wake mpya, ambapo mamia ya
wafanyakazi wahamiaji wanasafiri kwenda makwao kukutana na familia
zao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni