Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesera ( mwenye tai nyekundu ) akishiriki maandamano ya wiki ya mahakama mjini Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesera ( mwenye tai nyekundu ) akiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa wiki ya mahakama mjini Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesera akiongea wakati wa uzinduzi wa wiki ya mahakama mjini Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Mh. Richard Kasesera leo amezindua wiki ya mahakama kwa maandamano mjini Iringa yaliyoongozwa na brass band ya Magereza.
Akihutubia Majaji pamoja na wananchi amesisitiza uharaka wa kutoa HAKI, huku akisema kesi nyingi zinachelewa kuisha na wananchi wengi wamedhulumiwa haki yao na huu ni uvunjwaji katiba.
Pia amesisitiza wakina mama wasimamiwe haki zao. Kasesela pia alisisitiza polisi na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wakae pamoja kubaini kwa nini kesi nyingi ushahidi unakuwa haujakamilika na kuwataka wakamilishe ushahidi kabla ya kufungua kesi.
Bila haki nchi haiwezi kuendelea hata kidogo. Akitoa salamu zake Jaji Mfawidhi kanda ya Iringa Mh Mary Shangali aliahidi kuharakisha kesi pia kutembelea magereza yote ili kubaini waliocheleweshewa haki zao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni