Mpango wa Kijamii wa Uzalishaji Salama ili kusaidia kaya masikini kupambana na umasikini (PSSN) umefanikiwa kuwa na matokeo mazuri kwa kusaidia kaya Milioni 1.1 nchini na kusaidia juhudi za serikali kupambana na umasikini.
Hayo yamefahamika wakati washirika wa maendeleo ambao ni Umoja wa Mataifa, Benki Kuu ya Dunia, Serikali ya Uingereza kupitia kitengo cha Maendeleo ya Kimataifa, Irish Aid, USAID, Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Sweden (SIDA) walipotembelea miradi ya maendeleo katika wilaya za Unguja, Chamwino, Babati, Sumbawanga (Manispaa na Wilaya), Singida na Hanang kwa kipindi cha siku tatu kuanzia Januari, 19 hadi 22.
Bi. Kazijya Kila ambaye ni mmoja wa wanufaikaji wa fedha akitoa ushuhuda kuhusu mradi wake wa chakula ulivyowezeshwa na TASAF ambapo hadi hivi sasa anatengeneza faida ya Shilingi 7000 kwa siku na kabla ya kuwezeshwa alikuwa akikaa nyumbani na mama yake bila kuingiza kipato chochote.
Katika Mpango huo ambao utekelezwaji wake unasimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) unafanyika Tanzania Bara na Tanzania visiwani ukiwa na lengo la kuzisaidia kaya masikini pesa za matumizi ili kukidhi mahitaji ya kupata chakula pamoja na kuwawezesha kusaidia watoto wao kupata elimu jambo ambalo linaonekana kuzaa matunda kwa maeneo mengi ikiwepo Tanzania visiwani.
Serikali ya Tanzania imekuwa ikisaidia na washirika wa maendeleo ili kupunguza umaskini uliokithiri kwa wananchi wake na mwaka 2013 iliweka mpango wa kusaidia kaya masikini 275,000 kwa kipindi cha miaka mitano na tangu ianzishe mpango huo ilifanikiwa kusaidia kaya 275,000 kwa mwaka 2013 pekee katika wilaya nane nchini.
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed (kushoto) na Msimamizi wa mpango wa PSSN, Bw. Ramadhani Madari wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu kwa wanufaikaji wa fedha hizo.
Na mpaka kufikia sasa mpango huo umeshatoa malipo mara 12 na jumla ya kaya masikini milioni 1.1 zimeshafaidika na mpango huo ikiwa ni kwa wilaya 161 na vijiji 9789 nchini.
Malengo ya serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa ni kuhakikisha kufikia mwaka 2030 kunakuwa hakuna masikini hivyo ni wajibu wa kila nchi kuhakikisha inawasaidia wananchi wake ili wajijengee uwezo wa kujitegemea na kuondoka katika janga la umasikini.
Asilimia kubwa ya wanufaikaji wa mpango huo ni wanawake, kama wanavyoonekana pichani.
Mkurugenzi wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus Kamagenge akizungumza na wanufaikaji wa mpango wa TASAF (hawapo pichani).
Mkurugenzi wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus Kamagenge (kushoto) akifurahi jambo na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed.
Timu ya TASAF na wadau wa maendeleo wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo.
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed na Aine Mushi wa UN/NRA.
Bi Jabo Omari Othman akiwa kwenye shamba lake alilonunua kutokana na fedha za TASAF visiwani Unguja.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni