Mpishi Benoit Violier ambaye hoteli
ya Uswizi ilimtaja kama mpishi bora duniani Desemba mwaka jana
amekutwa akiwa amekufa nyumbani kwake.
Bw. Violier, 44, anaendesha hoteli
ya de l'Hotel de Ville huko Ctissier karibu na mji wa Lausanne.
Hoteli hiyo ilipata hadhi ya nyota
tatu na kuwa namba moja katika viwango vya dunia kati ya hoteli bora
1,000.
Polisi wa Uswizi wamesema Bw.
Violier, ambaye amezaliwa Ufaransa inaonekana amejiuwa kwa kujipiga
risasi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni