.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 2 Februari 2016

WANANCHI WA JIMBO LA BUMBULI WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA NI BAADA YA SERIKALI KUVUNJA MKATABA NA MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA KUZALISHA CHAI MPONDE


SERIKALI  ya  Tanzania  imevunja  rasmi mkataba  na mwekezaji
wakiwanda cha kuzalisha Chai cha Mponde kilichopo wilayani Bumbuli
Mkoani Tanga  na  kuamuru kitwaliwe   na kianze  kazi mara moja.

Akizungumza  katika  mkutano  uliowajumuisha  wadau  wazao  la
chai,Msajili  wa  Hazina  Laurence  Mafuru  amesema kuwa  kwa  mamlaka
aliyopewa  amevunja  rasmi mkataba huo   kwasababu  Mwekezaji
aliyekuwepo  kashindwa  kutekeleza  makubaliano  yaliyoweka .

Mafuru  alisema kuwa wamefikia  uwamuzi  huo  kutokana  na
kujiridhisha pamoja  na kupitia  mikataba  walioingia  na  mwekezaji
huyo  ndipo serikali imeamua  ikirudishe  kiwanda  hicho  mikononi
mwa  Wizara  ya Viwanda na Biashara  ili utaratibu  mpya wa
uendeshwaji  wa  kiwanda  uanze huku  Bodi ya Chai  Tanzania
ukiendelea  kukisimamia  mpaka  hapo  serikali itakapotafuta mwekezaji
 mwingine.

Mei mwaka 2013, wakulima wa chai waliitisha mkutano na kumwalika
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Januari Makamba na kueleza kutokuwa na
imani na mwekezaji na Chama cha Wakulima  wa Chai cha Usambara (UTEGA) na kuamua kukifunga kiwanda licha ya Mbunge kuwasihi wasichukue uamuzi huo wa hasira.

Tangu wakati huo jitihada nyingi zimefanyika zikiongozwa na Mheshimiwa
Makamba kuhakikisha kwamba kiwanda kinafunguliwa na wakulima wanauza
chai yao.

‘’ Tuliteseka  kwa  muda  mrefu  na  leo  Serikali  imefanya  uamuzi
wa kukirudisha  kiwanda  mikononi  mwetu, Tunaishukuru Serikali kwa
kutusaidia  sisi wananchi  tulioteseka  kwa muda mrefu ,” Alisema
Challes Ngovi  ambaye  ni mkulima wa  chai Mponde.


Hata  hivyo Mafuru  alibainisha  kuwa  ucheleweshaji wa kukifungua
kiwanda hicho  ulitokana na utaratibu  uliokuwa  ukifanywa na Serikali
 na  baada ya   kujiridhisha  ndipo  ikaamua  kumuandikia  rasmi
barua  Mwenyekiti  wa Utega  inayoonyesha  kuvunjwa  kwa mkataba  huo
na kuamuru kiwanda kirudi Serikalini.

Kwa upande wake, Mbunge  wa Bumbuli January Makamba  alisema kwamba
kazi waliyomtuma wananchi ya kukirudisha kiwanda mikononi mwao
imekamilika  ingawa imechukua muda mrefu.

Makamba  ambaye   pia ni Waziri Ofisi  ya Makamu  wa Rais
anayeshughuliokia  Mazingira  na Muungano alitumia  nafasi  hiyo
kumshukuru Rais   wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Magufuli  kwa
kuingilia kati  mgogoro huo  ambao  umedumu kwa zaidi  miaka  mitatu
na hatimae  kuumaliza.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Chai Usambara UTEGA
William Shelukindo aliilaumu serikali kutoka na uamuzi wake wa
kukitaifisha kiwanda hicho bila ya kutoa nafasi kwa mwekezaji kuweza
kujitetea kwani ni ameshindwa kuzalisha.

“Serikali katika hili imeshindwa kutupa nafasi ya kujitetea ili kuweza
kujua sababu za kushindwa kuzalisha ,lakini kwa sasa hatuna cha
kufanya zaidi ya kutekeleza matakwa yao”alisema Shelukindo.

 Ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alisema kuwa siku 90 za
kupeleka malalamiko na utetezi kwa seriklai zilishatangazwaa na
kumalizika kilichobaki ni utekelezaji wa kanuni na taratibu za
serikali kukichukuwa kiwanda na kuanza uzalishaji .

“Niwaombe wananchi hakikisheni mnazalisha zao hilo kwa wingi ili
kiwanda kiweze kufanyakazi na kuboresha uchumi wa kila mmoja
wenu,wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla kwani Bumbuli mnategemea zao la
chai kwa kiasi kikubwa.

Wakati huo huo,Wananchi waishio maeneo mbalimbali katika Jimbo la
Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga wamempongeza Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira kwa
hatua ya kuwasaidia kuishawishi serikali kukipatia ufumbuzi mgogoro wa
kiwanda cha chai cha Mponde.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi, mmoja ya
wakulima hao,Swahiba Mbili alisema kuwa kufunguliwa utawasaidia
wananchi ambao walikuwa na changamoto ya mazao yao kuharibika shambani
kupata soko la uhakika ambalo linaweza kuwainua kimaisha.

Swahiba alisema kuwa wao kama wakulima pamoja na kuishukuru serikali
kutwaa kiwanda lakini wanamshukuru Januari Makamba kwa sababu hakuweza
kuwa mbali nao kwenye kipindi chote wakati kiwanda hicho kimefungwa na
kuaidi kumpa ushirikiano katika kipindi cha kuwatumikia wananchi hao.

Mwisho.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni