Watumishi wa afya wamekuwa
wakipulizia dawa kwenye nyumba, shule pamoja na makaburini Amerika ya
Kusini, katika harakati za kujaribu kudhibiti kusambaa kwa virusi vya
Zika vilivyotangazwa leo kuwa janga la kiafya dharura duniani.
Shirika la Afya Duniani (WHO)
limesema mlipuko wa ugonjwa huo ni tatizo la kiafya la dharura
Kimataifa na kuuweka ugonjwa huo unaosambazwa na mbu katika daraja
moja na ugonjwa wa Ebola, uliouwa watu elfu 11 Afrika Magharibi.
Shirika la Afya Duniani limekadiria
kuwa watu wengi wanaoweza kufikia milioni 4 wataambukizwa na virusi
vya Zika mwaka huu.
Mtumishi wa Afya huko Lima akipulizia dawa makaburini kuuwa mazalia ya mbu
Mtoto aliyezaliwa na kichwa kidogo kutokana na maambukizi ya virusi vya Zika
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni