Kocha wa Inter Milan Roberto Mancini
amefungiwa mchezo mmoja baada ya kuonyesha ishara ya matusi katika
mchezo wa jumapili wa mahasimu wa soko wa Milan.
Kocha huyo wa zamani wa Manchester
City alishindwa ustaarabu baada ya Inter kuchapwa mabao 3-0 na AC
Milan katika mchezo wa Serie A.
Mancini alikasirishwa na kitendo cha
timu yake kunyimwa penati wakati wa kuwania mpira baina ya kipa wa AC
Milan Gianluigi Donnarumma na mshambuliaji wa Inter Milan Eder.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni