Mshambuliaji Luis Suarez amefunga goli katika
mchezo wake wa kwanza na timu yake ya taifa tangu afungiwe kwa
kumg'ata Giorgio Chiellini katika michuano ya kombe la dunia mwaka
2014.
Goli la Suarez liliisaidia Uruguay kutoka sare ya
mabao 2-2 dhidi ya Brazil katika mchezo ambao wenyeji Brazil walikuwa
wakiongoza kwa mabao 2-0, kabla ya Edison Cavani kurejesha goli moja
na Suarez kusawazisha la pili.
Renato Agusto akiifungia Brazil bao la pili katika mchezo huo
Wachezaji wa Barcelona Luis Suarez na Neymar wakikumbatiana kabla ya kuanza mchezo huo wa Brazil na Uruguay
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni