Mmoja wa wanafunzi wanaoshiriki mafunzo ya watoto yanayo endeshwa na shirika la Compassion International, Irene Lyandala akisoma risala
Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini, Richard Kasesela akifungua mafunzo hayo
Sehemu ya watoto wanaoshiriki mafunzo ya watoto yanayoendeshwa na shirika la Compassion International wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela
Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini, Richard Kasesela akifuatilia mafunzo hayo kwa umakiniJana Ijumaa Kuu tarehe 25/03/2016, mkuu wa wilaya ya Iringa mjini, Richard Kasesela ameshiriki katika uzinduzi na mafunzo ya watoto yanayo endeshwa na shirika la Compassion International (shirika la kikistro ambalo lipo nchi 28 duniani)
Shirika hili linahudumia zaidi ya watoto 4000 wa madhehebu yote mkoani Iringa. Mafunzo yatolewayo ni pamoja na;
1. Ulinzi wa Mtoto
2.Taarifa sahihi kuhusu VVU na UKIMWI
3.Ukombozi wa kiroho
4.Urafiki na urafiki wa siri
5.Ujasiliamali
6. Kulea maono
7.Stadi za Maisha
8. haki na wajibu wa Mtoto
9. Huduma na msaada wa Kisaikolojia
10. Kupambana na unyanyasaji na ukatili wa watoto.
Aidha mkuu huyo wa wilaya ya Iringa ametoa rai kwa wazazi kushiriki katika masomo na kulea vipaji vya watoto.
Amewashauri waunde vikundi ambavyo vitawafundisha uongozi na ujasiliamali na ila kikundi kiwe na watoto 20.
Amewaambia waandae wazo ambapo kikundi chenye wazo zuri kitapata laki 1 (vikundi 5 vitachaguliwa)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni