Mtuhumiwa wa mashambulizi ya Paris Salah Abdeslam amekataa
kuongea kuhusiana na mashambulizi ya jumanne Jijini Brussels,
Waendesha mashtaka wa Ubelgiji wamesema.
Wamesema kuwa Abdeslam aliyekamatwa wiki iliyopita Brussels na
kutoa ushirikiano hapo wa awali, ameamua kutumia haki yake ya kukaa
kimya na kukataa kusema lolote alipohojiwa kuhusu tukio hilo.
Salah Abdeslam alikamatwa siku chache kabla ya mashambulizi ya
Brussels, yaliyouwa watu 31.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni