Waendesha mashataka nchini Ubelgiji wamemfungulia
mashtaka ya ugadidi mwanaume mmoja kwa kuhusika na mashambulizi ya
jumanne Jijini Brussels yaliyouwa watu 28.
Mtuhumiwa huyo ametajwa kuwa ni Faycal C,
alikamatwa katika msako uliofanyika siku ya Alhamis, Jijini Brussels.
Katika mashambulizi hayo nusu ya majeruhi walikufa
kwenye uwanja wa ndege na wengine katika shambulizi la stesheni ya
treni. Kundi la Dola ya Kiislam (IS) limekiri kuhusika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni