Bondia Muingereza Kell Brook ametetea vyema mkanda wake wa IBF
wa uzito wa welterweight kwa kupata ushindi katika raundi ya pili
dhidi ya Kevin Bizier huko Sheffield hapo jana.
Brook, 29, alianza kwa kutumia nguvu zaidi dhidi ya mpinzani
wake huyo bondia wa Canada, na kufanikiwa kutetea taji hilo kwa mara
ya tatu mfululizo, tangu alitwae mwaka 2014.
Wakati huo huo Bingwa wa Olimpiki Luke Campbell alimshinda Gary
Sykes na kutwaa taji la Jumuiya ya Madola.
Bondia Kelly Brook akipambana na Kevin Bizier aliyeteleza chini
Bondia Kelly Brook akitupa konde la kulia lililomkalisha kwenye kamba Bizier
Bondia Kelly Brook akinyanyuliwa mkono juu baada ya kutangazwa mshindi wa pambano hilo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni