Timu ya Taifa ya Uingereza imetoka nyuma na kuweza kuwafunga
mabingwa wa Kombe la Dunia Ujerumani kwa maboa 3-2, huku kizazi kipya
cha Uingereza katika soka kikifanya vizuri katika mchezo huo
uliopigwa Jijini Berlin.
Katika mchezo huo Ujerumani ilionekana kama itaharibu mipango
ya Uingereza kung'ara kwa magoli yaliyofungwa na Toni Kroos la shuti
la masafa na kumshinda kipa Jack Butland, na baadae Mario Gomez
kufunga la pili kwa kichwa.
Dele Alli alicheza vyema na kumuunganishia Harry Kane
aliyepachika bao na Jamie Vardy akafunga goli lake la kwanza katika
mchezo wa kimataifa kutokana na krosi ya Nathaniel Clyne na Eric
Dier akapachika la tatu kwa kichwa.
Mpira uliopigwa na Gomez ukimpita kipa wa Uingereza Jack Butland
Jamie Vardy akituliza mpira kati kati ya mabeki wa Ujerumani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni