![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7a5ORG4Z3HGTwDu_bp1EUdQG68kHtXMhyphenhyphenA-xJMfAuMICfjamaU5jY3rhIRtBrGPOOB8E2Upt4qUelmJGU6CdPR8slgwhj-OETW_DMx93Gl_tgQzc4TCndHS3KQTA82tDvLXM1uBGSOKqR/s1600/NAIBU+WAZIRI+TAMISEMI++KASIMU+MAJALIWA.jpg)
Woinde shizza,Arusha
SERIKALI ya awamu ya tano imesema kuwa itaendeleza jitihada za kutunza na kulinda urithi wa dunia ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi maeneo ya uhifadhi ili watanzania wote waweze kunufaikana rasilimali za nchi .
Hayo yalisemwa na waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo
endelevu unaoendelea jijini Arusha
Majaliwa alisema kuwa rasilimali zilizopo ni za watanzania na ili kuhakikisha kuwa wananufaika nazo serikali itahakikisha inatunza na kulinda uhifadhi ili yawe endelevu na kusaidia vizazi vijavyo.
Alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi tajiri yenye urithi na hivyo ili kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika haswa waishio maeneo ya uhifadhi
serikali itatoa elimu ya kutosha ili waepuke kuchangia uharibifu wa mazingira
unaotokea kwenye hifadhi za taifa .
“Rasilimali hizi ni zetu na hivyo hata wanaoishi maeneo ya hifadhi
watusaidie kwa wale wanaoingilia na kuharibu kwani hata hizo mali asili zinatusaidia sote na ndiyo sababu tumewekea mikakati ya kutunza maeneo
hayo ili yawe endelevu’alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi Alisema kuwa
madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo
yanatishia na kuathiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia katika afrika .
Aidha mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kupitia upya shughuli
zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa
miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.
Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi
wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi
wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku
inayotokea kwenye maeneo ya urithi wa dunia kutokana na makundi ya
kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.
Aliongeza kuwa pia mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO ya
mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa
uridhi wa dunia.
“mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia utakuwa na
manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa bali
pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageni watakao
huthudhuria mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na
kujenga mitaji wa kijamii”alisema Malinzi
Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa
na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote
za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa
ya Ngorongoro
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni