Leo ni siku ya maamuzi kwa Makocha
wa Mataifa ya Ulaya kutangaza vikosi vyao vitakavyoshiriki michuano
ya Mabingwa wa Ulaya, Euro 2016, kabla ya muda wa kufanya maamuzi
hayo haujamalizika usiku.
Mataifa 24 yatashiriki michuano hiyo
ya kipindi cha majira ya joto, yote yatalazimika kuthibitisha vikosi
vyao vya wachezaji 23 mwisho ikiwa ni saa tano usiku, ambapo pia
kibarua hicho pia wanacho makocha wa mataifa ya Uingereza, Wales na
Jamhuri ya Ireland.
Kocha wa timu ya Uingereza almarufu
kama Simba Watutu, Roy Hodgson, anahitaji kupunguza kikosi chake huku
Fabian Delph akiwa imefahamika hatakuwemo, wakati wachezaji Ross
Barkley, Andros Townsend, Danny Drinkwater na Marcus Rashford
wakitarajiwa kuwamo.
Kinda wa Manchester United Marcus Rashford
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni