Mtumishi wa posta ambaye anafanana
mno na Jamie Vardy amezuiliwa na nyota huyo wa Uingereza kuwasiliana
naye kwenye mitandao ya jamii, na anaweza kushtakiwa iwapo atafanya
jambo litakalochafua heshima ya mshambuliaji huyo.
Shabiki huyo wa muda mrefu wa
Leicester City Lee Chapman, 29, amejikuta akiwa maarufu kutokana na
kufanana mno na Vardy, ambapo pia alimkaribisha kwenye basi la timu
hiyo kusherehekea ubingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Lee Chapman kulia akiwa na Jamie Vardy
Lee Chapman akiwa na shabiki mwingine anayefanana pia na Jamie Vardy
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni