.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 25 Mei 2016

MFUMO WA USIMAMIZI WA NYARAKA KIDIJITI KUONGEZA KASI YA UTENDAJI SERIKALINI

mo1 
Katibu mkuu wizara ya habari,utamduni,sanaa na michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo wakati menejimenti ya wizara hiyo ilipofanya ziara ili kujifunza mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijitali unavyofanya kazi katika ofisi za wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano leo jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora na Naibu katibu mkuu wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo Bi.Nuru Khalfan Mrisho.
mo2
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora akieleza jambo kwa menejiment kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo walipofika ofisini hapo ili kujifunza mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijitali.
mo3
Watumishi pamoja na Menejimenti kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Kaimu mkuu wa masijala ya wazi Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Bi.Bupe Munisi(wa kwanza mwenye nguo ya njano) jinsi mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijiti(DMIS) unavyofanya kazi .
mo4Menejimenti ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakiwa katika ziara mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijitali unavyofanya kazi katika ofisi za wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano.

 

Na Daudi Manongi.

Mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijiti utaongeza kasi serikalini na hivyo kuchochea maendeleo chanya katika kila nyanja.

Hayo yamesemwa leo na Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel wakati wa mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kwa Menejimenti ya wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati walipotembelea mfumo wa usimamizi wa nyaraka wa kidijiti.

Alisema pia kuwa mfumo huu una faida nyingi na ndio ambazo zimeifanya wizara hii kutaka kujifunza ni pamoja na suala la gharama na kwa kuwa serikali ya awamu ya tano iko katika jitihada kubwa za kupunguza matumizi na kwa kuwa bajeti ya shajala ni kubwa katika taasisi nyingi za serikali hivyo mfumo huu wa kidijiti utasaidia kupunguza garama kwani hapatakuwa na haja ya kutumia karatasi na hivyo kupunguza gharama kubwa.

Prof Elisante pia aliongeza kuwa mfumo huu utaongeza usiri wa nyaraka hizi na kwa sasa zitakuwa zinasomwa na yule tu aliyekusudiwa na kutoa pongezi kwa ofisi ya rais manejimenti ya umma kwa kuhamasisha matumizi ya mfumo huu kwani ukitumiwa vyema utakuwa na manufaa sana.

Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora alisema kuwa mfumo huo ulijengwa miaka mitatu iliyopita na unaweza kutumika katika wizara yeyote kwani una ufanisi mkubwa sana kwani kwa sasa utaweza kuangalia mafaili gani yameingia kwa mfumo wa kidijitali na kwa namna hii itapunguza garama na muda kwani hatutakuwa tunatumia karatasi tena.

Prof.Kamuzora alizitaka Taasisi na Wizara mbalimbali kuwapa elimu ya kutosha watunza kumbukumbu kwani wao ndio wahusika wakuu wa kwanza wa mfumo huu na hivyo kuwataka wahusika kuwapa mafunzo ya kompyuta na kuboresha vifaa kama scanner maofisini mwao.

Nae mmoja wa watunza kumbukumbu kutoka wizara Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Felomena Swai alisema amenufaika na mafunzo hayo na yatawasaidia katika utunzaji wa kumbukumbu kwani sasa watapeleka barua kwa wakati na kurahisisha utunzaji wa mafaili.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni