Kamanda wa Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi
Baada ya siku sita tangu waumini wawili akiwamo Imamu wa msikiti wa Rahmani, Feruzi Eliasi, uliopo Ibanda Relini Kata ya Mkoloni jinamizi la mauaji hayo mkoani Mwanza limezidi kutisha baada ya jana usiku, Mwenyekiti wa mtaa wa Bulale kata ya Buhongwa, kuuawa kwa kupigwa risasi.

Tukio
hilo lililotokea juzi saa 2 usiku, lilimkumba Mwenyekiti huyo,
Alphonce Mussa (48), mkazi wa Bulale kata ya Buhongwa wilaya ya
Nyamagana jijini Mwanza, aliyepigwa risasi mbili na watu wawili
wasiojulikana wakati akijaribu kusuluhisha mgogoro wa ndoa kati ya
Neema Marangula na mumewe.
Akisimulia
tukio hilo kwa majonzi huku akiangua kilio, mke wa marehemu, Getrude
Henrico, alisema wakati tukio hilo linatokea hakuwepo nyumbani kwani
wakati huo alikuwa bustanini, alisimuliwa tukio hilo alipofika
nyumbani.
Hata
hivyo, mjane huyo alisema kabla ya tukio hilo, siku za karibuni
waliuwa mbwa wao saba waliokuwa wanalinda mifugo, hivyo anahisi tukio
hilo la mauaji ya mumewe yanaendana kabisa na kuuliwa kwa mbwa hao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni