JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail:
press@ikulu.go.tz
Tovuti :
www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kabla
ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la
Mawaziri (Cabinet
Clerk).
Bw.
Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye
amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Wakati
huo huo,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya
uchumi.
Kabla
ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi
katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo tarehe 23
Mei, 2016 imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es salaam
23
Mei, 2016
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni