SIKU chache baada ya pazia la ligi kuu ya soka Tanzania bara
kufungwa,Kocha mkuu wa Mbeya City Fc Kinnah Phiri ameanza zoezi
maalumu la kusaka nyota wapya ambao atawajumuisha moja kwa moja kwenye
vikosi vya timu yake msimu ujao.
Akizungumza muda mfupi baada ya majaribio ya siku ya kwanza kwa
wachezaji wapya vijana waliofika kujaribu bahati zao kwa kuonyesha
vipaji walivyonavyo navyo, afisa habari wa City Dismas Ten amesema kuwa
muitikio umekuwa mzuri katika siku hii kwanza ambayo nyota hao wa
baadae wamefika kuonysha uwezo wao mbele ya kocha huyo raia wa malawi.
“Leo ni siku ya kwanza, kitu kizuri mwitikio umekuwa
mkubwa, takribani vijana 50 wamejitokeza kujaribu bahati zao kulingana
na vipaji walivyonavyo, haya ni majaribio ambayo kocha Phiri ameyaitisha
ili kusaka vipaji vipya ambavyo moja kwa moja vitaingia kwenye timu
yetu kubwa na ile ya U20, alisema.
Akiendelea zaidi, Ten alisema kuwa, hii imekuwa ni kawaida kwa
City kila inapofika mwisho wa msimu kuwaleta pamoja vijana wote
wanaoamini wanauwezo wa kucheza mpira, kufichua vipaji vyao ili waje
kuwa wachezaji wakubwa baadae.
“Hii ni kawaida yetu, kila tunapomaliza msimu huwa
tunafanya hivyi, vijana wote wenye umri kuanzia miaka 17-22 ni fursa
kwao kujitokeza, zoezi hili la kusaka vipaji litakuwepo kwa juma zima,
leo hatukuwa na kocha Phiri kwa sababu alikuwa kwenye majukumu mengine
lakini kesho tutakuwa kwenye uwanja Sokoine na mwalimu atakuwa, kwa
hiyo vijana wote ndani ya jiji la Mbeya na mikoa ya jirani waje kujaribu
bahati zao.
Kwa upande wa vijana waliojitokeza siku ya leo, walishukuru kuwepo kwa
zoezi hili kwa sababu limerahisisha uwezekano wa vipaji walivyonavyo
kuonekana mapema hatimaye waweze kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji
wakubwa siku za usoni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni