Mgomo wa kupinga sheria
mpya za kazi nchini Ufaransa umesambaa katika mitambo yote minane ya
kusafishia mafuta ghafi umoja wa wafanyakazi umesema na kukuza
mgogoro na serikali.
Kutokana na kufungwa
kwa njia za kwenda kwa mitambo ya kusafishia mafuta ghafi asilimia 20
ya vituo vya mafuta nchini Ufaransa vimeishiwa na mafuta kutokana na
kukosa mafuta yanayoingizwa.
Waziri Mkuu wa
Ufaransa, Manuel Valls, amesisitiza sheria za kazi mpya
hazitaondolewa, na vikosi vya usalama vitayasambaratisha makundi
yanayozuia njia za mitambo ya kusafishia mafuta.
Polisi wakihangaika kuondoa kizuizi katika moja ya barabara ya mtambo wa kusafishia mafuta ghafi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni