Mcheza soka wa
Uingereza Jamie Vardy anatarajiwa kumuoa mchumba wake kwa harusi ya
kifahari itakayofanyika hapo kesho.
Kwenye harusi ya
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, mpambe wa kiume atakuwa David Nugent, katika
harusi hiyo itakayofanyika Peckforton Castle, huko Cheshire.
Hata hivyo harusi hiyo
haitohudhuriwa na mama yake mzazi pamoja na baba wa kambo ambao
hawamkubali mkwe wao huyo mtarajiwa Becky Nicholson.
Jamie Vardy akiwa ameshikilia kombe la Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na mchumba wake
Baba wa kambo wa Jamie Vardy, Phil hatohudhuria harusi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni