Magoli ya dakika za mwisho ya
Antoine Griezmann na Dimitri Payet yamewahakikishia wenyeji wa
michuano ya Euro 2016 timu ya Ufaransa ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya
Albania na kutinga hatua ya mtoano.
Katika mchezo huo Albania walikuwa
wa kwanza kugonga mwamba wa goli la Ufaransa katika kipindi cha pili
baada ya Ledian Memushaj kupiga krosi iliyompita kipa wa Ufaransa
Hugo Lloris.
Dimitri Payet akipiga shuti la kuzungusha lililojaa wavuni
Dimitri Payet akiruka juu na kukanyaga kibendera cha kona akishangilia goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni