Mchezaji Marek Hamsik amefunga goli
la dakika za mwisho na kuifanya Slovakia kuwafunga Urusi kwa magoli
2-1 na kupata ushindi wao wa kwanza katika michuano ya Euro 2016.
Katika mchezo huo kiungo huyo wa
Napoli alitoa pande kwa Vladimir Weiss ambaye alipiga mpira kwa
kuuchonga na kuifanya Slovakia kuongoza kwa goli moja. Urusi walipata
goli la kufutia machozi kupita kwa Denis Glushakov.
Marek Hamsik akiachia shuti lililozaa goli la pili kwa Slovakia
Kipa wa Slovakia akiruka bila ya mafanikio kuzuia mpira usiingie wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni