Chama cha Jubilee na kambi ya
upinzani ya CORD jana wamekubaliana kuanza mazungumzo majadiliano
kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, jambo ambalo litasaidia
kupunguza mvutano baina ya serikali na upinzani.
Makubaliano hayo yamefikiwa Ikulu
Jijini Nairobi, kati ya rais Uhuru Kenyatta, Naibu rais William Ruto
na kwa upinzani viongozi wa CORD wakiwakilishwa na Raila Odinga na
Moses Wetang’ula.
Mkutano huo pia uliondoa mvutano wa
kuwa na mikutano miwili ya sherehe za Siku ya Madaraka, ambapo Rais
Uhuru Kenyatta alimualika Raila Odinga katika maadhimisho ya kitaifa
ya Siku ya Madaraka Nakuru kwenye Uwanja wa Nakuru hii leo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni