.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 1 Juni 2016

MRACUS RASHFORD ANA UMRI MDOGO KULIKO WACHEZAJI WOTE WA EURO 2016

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, anakuwa ni mchezaji mwenye umri mdogo kuliko wote katika vikosi vyote 24 vya mataifa yanayoshiriki michuano ya Euro 2016, itakayochezwa nchini Ufaransa

Mshambuliaji huyo kinda aliyeitwa kuchezea kikosi cha taifa cha Uingereza katika michuano hiyo ana miaka 18 na siku 214, ambapo anayemfuatia kwa udogo kwenye michuano hiyo ni Renato Sanches, wa Ureno aliyemzidi kwa miaka 18 miezi miwili.

Kwa ujumla katika michuano ya Euro 2016 timu ya taifa ya Uingereza inawachezaji wenye umri mdogo wengi wa chini ya miaka 23, kuliko vikosi vyote vinavyoshiriki michuano hiyo kutokana na kuwa na wachezaji saba.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni