Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela akiongea jambo katika hafla hiyo.
Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela alikuwa Mgeni rasmi katika changizo la kwaya Kuu ya KKKT Kihesa hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Iringa.
Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela alikuwa Mgeni rasmi katika changizo la kwaya Kuu ya KKKT Kihesa hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Iringa.
Iliongozwa na Baba Askofu O.M. Mdegela ambapo Kiasi cha shilingi 8,950,000 zilichangishwa.
Mungu alitenda muujiza wa utoaji. Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya aliomba sana wakristo waliombee taifa hasusani Wilaya ya Iringa ambapo watoto wamekuwa wananyanyaswa sana kijinsia.
Baba askofu katika mahubiri yake aliwaomba waumini kuimba nyimbo kwa staha na pia kuangalia ni nani wanaye mwimbia. hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wakuu wa majimbo na wachungaji pamoja na viongozi wengine wa serikali na vyama.
(Kwa habari zaidi pia tembelea IRINGA DC FACEBOOK PAGE)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni