Watu wapatao 10 wakiwemo wabunge
wawili wameuwawa katika mlipuko uliotegwa kwenye gari pamoja na
mashambulizi ya silaha jana katika hoteli moja kuu katika Jiji la
Mogadishu nchini Somalia.
Watu wengine 40 wamejeruhiwa katika
shambulizi hilo kwenye hoteli ya kati kati ya Mji ya Ambassador,
ambapo vikosi vya usalama vililazimika kupambana na wapiganaji wa
kundi la al-Shabaab kwa muda wa saa tano jana usiku.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni