Gwiji la Soka Pele amempatia ushauri
mmoja tu mchezaji kinda, Marcus Rashford, anayeelekea kucheza
michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa, kwa kumumbia neno moja tu
'Usiogope'.
Mkongwe huyo wa Brazil Pele aliitwa
kuchezea timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 16 na alishinda kombe
lake la kwanza la Dunia mwaka moja baadaye 1958.
Rashford, 18, alikuwa anachezea timu
ya taifa chini ya miaka 21 mwaka moja uliopita, lakini sasa amepanda
na anachezea timu ya wakubwa ya taifa ya Uingereza chini ya kocha Roy
Hodgson.
Marcus Rashford akiwa mazoezini na timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama Simba Watatu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni