Picha juu na chini ni Brass Band ikiongoza gwaride maalum la askari walinda Amani kuingia viwanja wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.Manyama.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa ambapo kwa nchini siku hiyo iliadhimishwa Dar es Salaam katika Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja
Manyama alisema Tanzania imekuwa ikijitolea kusaidia ulinzi wa amani katika mataifa mengine licha ya kupoteza baadhi ya wanajeshi wake lakini bado wamekuwa wakiendelea kujitolea kusaidia kuimarisha ulinzi wa mataifa mengine ambayo hali ya usalama inakuwa siyo ya uhakika.
“Tumefurahishwa na historia ya Tanzania ya kuzisaidia nchi jirani kulinda amani na kutatua migogoro ya hapo zamani na kuziwezesha kujipatia uhuru,” alisema Manyama.
Aidha Manyama alisema Umoja wa Mataifa umekuwa ukijitahidi kuendelea kushirikiana na wanachama wake ili kwezesha upatikanaji wa amani kwa mataifa yote na itaendelea kutoa heshima yake kwa wanawake na wanaume ambao walipoteza maisha wakiwa kazini kulinda amani ya mataifa mengine.
“Mwaka jana idadi ya waliokufa ilikuwa 129, walinda amani hawa walitoka katika nchi 50, wakiwa ni pamoja na wanajeshi, polisi, watumishi kutoka mataifa mbalimbali, wafanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa na watumishi wa ndani,
“Tunapenda kutoa heshima kwa mashujaa wetu zaidi wanaume na wanawake milioni moja waliotumikia chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa kwa majivuno, weledi tangu kuanza kwa kazi hiyo 1948,” alisema Manyama.
Nae mgeni rasmi katika siku hiyo, Meja Jenerali James Mwakibolwa aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa jinsi wanavyofanya kazi na kusaidia kuokoa maisha ya watu wengi na kuahidi Tanzania itaendelea kutoa wanajeshi wake ili waendelee kulinda amani.
“Tumeshatoa walinda amani 2,328 katika operesheni mbalimbali zilizopita na tutandelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha amani na utulivu katika maeneo mengine,” alisema Meja Jenerali Mwakibolwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni