Timu ya Manchester City imekamilisha
mpango wa kumnunua kiungo wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan kwa
kitita cha paundi milioni 21, na kumpa mkataba wa miaka minne.
Gundogan anakuwa mchezaji wa kwanza
wa Manchester City kusajiliwa na kocha mpya Pep Guardiola tangu
ajiunge na timu hiyo inayotumia dimba la Etihad.
Kiungo huyo wa kati mwenye miaka 25
anaondoka Borussia Dortmund baada ya kuichezea klabu hiyo mara 157.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni