Mchezaji wa Argentina na timu ya
Barcelona, Lionel Messi, anatarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama
nchini Hispania kwa makosa ya kukwepa kodi.
Messi na baba yake Jorge, ambaye
anasimamia masuala yake ya kifedha, wanashtakiwa kwa kukwepa kodi
Hispania ya dola milioni 4.5 kati ya mwaka 2007 na 2009.
Mamlaka za nchi hiyo zinadai kuwa
wawili hao walitumia kukwepa kodi kwa kuficha fedha katika mataifa
yasiyotoza kodi ya Belize na Uruguay.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni