Timu ya taifa ya Uingereza jana
usiku imemalizia maandalizi ya michuano ya Euro 2016 kwa ushindi
mdogo dhidi ya wachezaji 10 wa timu ya taifa ya Ureno, katika dimba
la Wembley.
Goli pekee la Uingereza lilipatikana
kupitia mpira wa kichwa uliopigwa na Chris Smalling akipokea mpira wa
krosi uliopigwa na Raheem Sterling.
Katika mchezo huo Ureno walijikuta
wakimpoteza Bruno Alves kwa kumchezea vibaya Harry Kane katika dakika
ya 35 kutokana na kunyanyua daluga lake juu kwenye kichwa cha Kane.
Chris Smalling akipiga kichwa mpira uliojaa wavuni na kuipa ushindi Uingereza
Bruno Alves akimfanyia rafu mbaya mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni