Mabingwa watetezi timu ya Golden
State Warriors wamewafunga Cleveland Cavaliers kwa vikapu 104-89
katika mchezo wa ufunguzi wa Fainali ya Ligi Kuu ya Kikapu ya
Marekani (NBA).
Wakati nyota Stephen Curry na Klay
Thompson wakiwa hawapo kwenye viwango vyao vya juu kimchezo Golden
State Warriors waliwategemea wachezaji wa benchi Shaun Livingston,
Andre Iguodala na Leandro Barbosa kuisaidia kuibuka na ushindi huko
Oakland.
Katika mchezo huo Livingston
alifunga pointi 20, Iguodala pointi 12 na Barbosa pointi 11, huku
Curry ambaye ni mchezaji ghali kuliko wote kwenye Ligi ya NBA na
Thompson kuambulia pointi 10 kila mmoja.
LeBron James akimkaba Stephen Curry katika mchezo huo wa fainali ya NBA
Mchezaji nyota Stephen Curry akiwa angani kufunga kikapu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni