.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 15 Juni 2016

MABONDIA GALILE NA MAPAMBANO KUMALIZA UBISHA JULAY 24 MUSOMA BAR



Mdau wa masumbwi nchini Jumanne Mbwembwe akiwainua mikono juu mabondia Imani Mapambano kushoto na Seleman Galile kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa julay 24 katika ukumbi wa musoma bar Tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Iani Mapambano kushoto na Selemani Galile wakiwa katika pozi wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa julay 24 katika ukumbi wa musoma bara tasndika Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Imani Mapambano kushoto akitunishiana misuli na Selemani Galile baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga julay 24 katika ukumbi wa musoma bar tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS


                                                                                                           Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Imani Mapambano na Selemani Galile wamesaini mkataba wa kuzipiga Julay 24 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika Dar es salaam


Akizungumza baada ya kusainishwa kwa mabondia hawo mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D'  amesema amewasainisha mabondia hawo baada ya kutambiana mara kwa mara kadri wakutanapo  hivyo nimeamua wapambane julay 24 katika ukumbi wa musoma bar ili kumaliza ubisha wao. 


Mpambano huo utakuwa wa ubingwa wa Taifa utakaosimamiwa na TPBO chini ya rais wake Yassin Abdallah 'Ustadhi'

Aliongeza kwa kusema kuwa mipambano mingine ya utangulizi watatangaza kadri watakavyo ingia mikataba na mabondia mbali mbali

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni