Umoja wa madjs wa zamani waliosumbua katika muziki wa Disco enzi zao ulikutana tena siku ya Jumanne June 14, 2016 Escape one Mikocheni katika kikao chao cha kamati iliyoteuliwa kuunda katiba ya umoja huo uliobeba jina la Tanzania Worldwide Djs ukiwa unawajumuisha madjs wote waliotamba enzi zao ambao kwa sasa wametapakaa kote dunia. Walioshiriki kikao maalum cha kutengeneza katiba ni Dj Saydou, Dj Godfather, Dj Peter Moe, Dj Ebony M, Dj Venture, Dj Young Ray na Dj Young Jesse.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni