Serikali ya Ufaransa imeisihi miji
ambayo michezo ya Euro 2016 inachezwa kupiga marufuku pombe karibu na
viwanja na makazi ya mashabiki wa mpira.
Kauli hiyo ya serikali ya Ufaransa
imekuja baada matukio ya siku tatu ya mapambano baina ya mashabiki na
polisi huko Marseille.
Shirikisho la Sola Barani Ulaya
(Uefa) linachunguza baada ya mashabiki wa Urusi kuonekana
wakiwakimbiza mashabiki wa Uingereza uwanjani na kuwapiga baada ya
kutoka sare ya goli 1-1. Pia Uefa imetishia kuzifungia timu za Urusi
na Uingereza iwapo zitasababisha ghasi zaidi.
Serikali ya Uingereza imesema ipo
tayari kutuma polisi wake wa ziada kuelekea mchezo wa Uingereza ujao
huko Lens utakaopigwa siku ya Alhamis.
Mashabiki wa Urusi wakiwashambulia mashabiki wa Uingereza wanaokimbia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni