Aliyekuwa mke wa mwanaume
aliyewafytulia risasi watu kwenye klabu ya usiku ya mashoga huko
Orlando Marekani majira ya asubuhi siku ya jumapili, amesema kuwa
mumewe huyo aliyetengana naye alikuwa na matatizo ya akili, na
alikuwa amechanganyikiwa.
Mtu huyo Omar Mateen aliwauwa watu
50, na kujeruhi wengine 53 ikiwa ni tukio baya la shambulizi kwa
umati wa watu katika historia ya Marekani katika siku za hivi
karibuni, hata hivyo naye aliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Kundi la kigaidi linalojiita kuwa
Dola ya Kiislam, limesema limehusika na shambulizi hilo, hata hivyo
uhusika wake wa moja kwa moja na tukio hilo, haujabainika wazi.
Kampuni ya ulinzi ambayo Mateen alikuwa anafanyakazi imesema
alifanyiwa mchujo mara mbili.
Muuaji Omar Mateen akiwa na aliyekuwa mkewe pamoja na mtoto wao
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni