Washindi mara tano wa Kombe la Dunia
Brazil, wamepoteza mchezo kwa kuchapwa goli 1-0 na Peru na kutupwa
nje ya michuano ya Copa America katika hatua ya makundi kwa mara ya
kwanza tangu kupita miaka 30.
Timu ya taifa ya Brazil haijawahi
kushindwa na Peru katika kpindi cha miaka 16 waliochokutana ilikuwa
inahitaji pointi moja tu ili kutinga robo fainali lakini ikajikuta
ikilala dhidi ya Peru.
Katika mchezo huo Raul Ruidiaz
aliyetokea benchi alifunga goli hilo pelee katika dakika ya 75,
kwenye dimba la Foxborough huko Massachusetts, ambalo Brazili
walilalamikiwa kuwa limefungwa kwa mkono.
Katika mchezo Ecuador iliifunga
Haiti 4-0 na kutinga hatua ya nane bora kwa mara ya kwanza tangu
mwaka 1997.
Raul Ruidiaz akifunga goli ambalo kama unavyoonekana mkono wake ukiwa karibu na mpira
Mpira uliopigwa na Ruidiaz ukitinga wavuni mwa goli la Brazil huku kipa akiwa kapotea mahesabu
Kipa wa Brazil akimlalamikia refa kwa kukubali goli analodai limefungwa kwa mkono
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni