Nchi
za Misri na Senegal zimefanikiwa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika
mwaka 2017 (AFCON) itakazochezwa nchini Gabon, kwa kupata ushindi
katika michezo yao iliyochezwa hii leo.
Winga
wa Roma Mohamed Salah alifunga magoli yote ya Misri katika ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania, na kurejea katika fainali
hizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010.
Timu
ya Senegal nayo ilikata tiketi ya kwenda Gabon mwaka 2017, shukrani
kwa magoli yaliyofungwa na wachezaji wa ligi kuu ya Uingereza, Sadio
Mane na Mame Biram Diouf, waliyoipatia magoli 2-0 dhidi ya Burundi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni