Papa
Francis ameridhia hatua za kuwatimu maaskofu ambao hawatosimamia
vyema kesi za matukio ya udhalilishaji kingono watoto ndani ya
dhehebu la Kanisa Katoliki.
Maaskofu
ambao wataonyesha uzembe katika kushughulikia kesi za mapadri
waliohusika na ukatili huo dhidi ya watoto, sasa wataondolewa chini
ya taratibu mpya za sheria.
Sheria
hiyo mpya imekuja wakati kukiwa na shinikizo kwa wahanga wa vitendo
vya udhalilishaji watoto, wakitaka kuchukuliwa hatua kwa maaskofu
wanaozembea kusimamia vyema ukatili huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni