Bw Conrad Mbuya ,Mkurugenzi wa Shughuli za Mikoa PS 3 akitoa maelezo Kwa washiriki toka Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi jinsi mradi utakavyo fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria Ofisi ya Rais TAMISEMI,Edwin Mgendera alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Lindi, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi pamoja na washiriki wengine wakiwa katika majadiliano ya Pamoja wakati wa Uzinduzi huoKatika kuimarisha Ubora wa Utoaji huduma za Umma na Matumizi yake kwa ajili ya Kuboresha na kuimarisha Mifumo,Mkoa wa Lindi Umezindua Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya sekta za umma utakaowezesha Jamii katika Ngazi ya halmashauri kutumia rasilimali kwa Uwazi na kuwezesha ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga na kufuatilia matokeo ya kila sekta
Mpango huo utakaosaidia utoaji wa ushauri wa kitaalamu na kuwajengea uwezo wafanyakazi ili kuongeza Usawa wa mgawanyo wa rasilimali watub kwa ajili ya utoaji bora wa huduma katika maeneo yenye Uhitaji zaidi ikiwemo mfumo wa ajira pamoja na kudumisha watumishi katika Ajira Serikalini
Akizindua Mradi huo wa PS 3,Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi amesema kuwa mradi huo wa uhimarishwaji wa mifumo ya sekta za Umma nchini utasaidia kuondoa tatizo sugu la watumishi hewa endapo utekelezaji wake utafanyika vizuri.
Awali akitoa taarifa katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mradi katika Mikoa, Dk.Conrad Mbuya alisema mradi huo utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.
Kufuatia Uzinduzi wa Mradi huo,Mkuu wa Wilaya ya Lindi Yahya Nawanda pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Abuu MjakA walieleza kuwa mradi huo pia utasaidia ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma ikiwemo ushirikishwaji wa Madiwani katika Utekelezaji wa mradi huo Utakaoboresha Utendaji na Uwajibikaji katika kutoa huduma kwa Jamii
Mradi huo uliozinduliwa leo unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania Bara ambayo ni Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma,Mara,Mbeya, Morogoro, Mtwara,Mwanza, Njombe, Rukwa na Shinyanga pamoja na Lindi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni